Mawaziri watano wa Serikali inayomaliza muda wake wameanguka kwenye uchaguzi majimboni mwao, sambamba na wagombea wengine maarufu wa Bunge lililopita baada ya matokeo ya kura zilizopigwa Jumapili kuanza kutangazwa jana.
Mawaziri hao wanaungana na wabunge wengine maarufu wa Bunge la Kumi walioshindwa kutetea majimbo yao, wakiwamo wa kambi ya upinzani ambao wameangushwa na wagombea wa CCM.
Pia wamo mawaziri wa zamani wawili, Cyril Chami na Omary Nundu walioanguka kwenye uchaguzi, kwa mujibu wa matokeo ambayo yanaendelea kutangazwa.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema jana kuwa itakamilisha kazi ya kutangaza matokeo yote keshokutwa.
Mawaziri walioanguka kwenye uchaguzi huo ni Steven Wasira, Christopher Chiza, Aggrey Mwanri, Dk Steven Kebwe na Anne Kilango.
Katika matokeo yaliyotangazwa jana, Wasira, kada maarufu na mwanasiasa mkongwe aliyekuwa akitetea Jimbo la Bunda, alijikuta akiangushwa na mwanasiasa kijana, Ester Bulaya, ambaye alihamia Chadema baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake.
Wasira, ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo na Chakula, alianza mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa kuomba ridhaa ya CCM agombea urais, lakini hakupitishwa. Bulaya, ambaye alikuwa mbunge wa viti maalum (CCM), alipata kura 28, 508 na kumuacha mbali waziri huyo mkongwe aliyepata kura 19, 126.
Mwingine aliyeanguka ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwezeshaji na Uwekezaji, Christopher Chiza ambaye ameangushwa na Bilago Samson wa Chadema katika Jimbo la Buyungu. Waziri huyo alizidiwa kwa kura 104 baada ya Samson kupata kura 23,041 dhidi ya 22,934 za Chiza.
Lakini hali haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Aggrey Mwanri kwenye Jimbo la Siha. Waziri huyo alizidiwa kwa zaidi ya kura 4,100 na mpinzani wake kutoka Chadema, Dk Godwin Mollel aliyepata kura 22,746.
Katika Jimbo la Serengeti, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe pia alijikuta akipoteza nafasi ya kurudi bungeni kwa kura alipoangushwa na Marwa Ryoba wa Chadema. Dk Kebwe alipata kura 39,232, akiwa amezidiwa na mpinzani wake kwa zaidi ya kura 820.
Anne Kilango, ambaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu mwaka 2013 baada ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyosababishwa na kashfa ya Operesheni Tokomeza, ameangushwa na mgombea wa Chadema, Naghenjwa Kaboyoko wa Chadema kwa tofauti ya kura 3,297.
Kilango alipata kura 15,539 wakati mgombea huyo wa Chadema alipata kura 18,836. Pia wabunge maarufu kama Vincent Nyerere (Musoma Mjini), James Lembeli (Kahama Mjini) na Kyisieri Chambiri (Babati Mjini) wameangushwa.
Nyerere, aliyekuwa akitetea kiti cha Musoma Mjini kwa tiketi ya Chadema, aliachwa mbali na mgombea wa CCM, Vedastus Mathayo aliyepata kura 32, 836 dhidi ya 25,549.43 za Nyerere.
Lembeli, ambaye alihamia Chadema muda mfupi baada ya Bunge la Kumi kumaliza muda wake, aliachwa mbali na mfanyabiashara maarufu, Jumanne Kishimba aliyepata kura 47,553 dhidi ya kura 30,122 za Lembeli.
Walioshinda
Wakati hao wakidondoka wabunge wengine wameendelea kutetea majimbo yao kwa kupata kura za kishindo, wakiongozwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyetetea jimbo lake la Hai, Joshua Nassar (Chadema, Arumeru Mashariki), Stephen Masele (CCM, Shinyanga Mjini), Jenister Mhagama (CCM, Peramiho), Silvestry Koka (CCM, Kibaha), David Silinde (Chadema,Momba), Aesh Hilaly (CCM, Sumbawanga Mjini), Joseph Selasini (Chadema,Rombo), Profesa Jumanne Maghembe (CCM Mwanga).
Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge (TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko (Chadema) 20,017, Michael Kembaki (CCM), 14, 025, Deogratias Meck (ACT-Wazalendo) 356.
Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Jimbo la Buyungu
Ubunge: Kasuku Bilago (Chadema), 23,041, Christopher Chiza (CCM) 22,934, Athanas Mawazo (NCCR-Mageuzi) 1,237 na Leopold Muahanga(ACT Wazalendo).
Jimbo la Lindi Mjini
Ubunge: Selemani Kaunje (CCM) 20,733 na Salum Barwany (CUF) 18, 843.
Jimbo la Mkinga
Ubunge: Dustan Kitandula (CCM) 21,623, Bakari Kassimu (CUF) 13, 547, Rachel Sadick (Chadema) 3,789 na Ali Mwita (ACT Wazalendo) 402.
Jimbo la Tandahimba
Ubunge: Ahmad Katani (CUF) 55,156, Shaibu Likumbo (CCM) 41,088 na Hamis Hassan (ADC) 966.
Jimbo la Mbinga Mjini
Ubunge: Sixtus Mapunda (CCM) 28,364 na Mario Milinga(Chadema) 102.
Jimbo la Mbinga Vijijini
Ubunge: Martin Msuha (CCM) 59, 269 na Benjamin Akitanda (Chadema) 11, 285.
Jimbo la Nzega Mjini
Ubunge: Hussein Bashe (CCM) 18,754, Charles Mabula(Chadema) 9,658, Kitwana Abdallah (ACT Wazalendo) 180 na Leonard John(CUF) 95.
Jimbo la Peramiho
Ubunge: Jenista Mhagama (CCM) 32,057, Mwingira Erasmo (Chadema) 11,462 na Claudius Claudius(DP) 217.
Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge: Vedastus Mathayo (CCM) 32, 836, Vincent Nyerere (Chadema) 25, 549, Esseko Tongola (ACT Wazalendo) 513, Gabriel Ocharo (CUF) 186, Maimuna Matola (ADC) 50, Ibrahim Selemani (Tadea) 21, Rutaga Sospeter (AFP) 25 na Makongoro Jumanne (UMD) 19.
Jimbo la Geita Mjini
Ubunge: Kanyasu John (CCM) 34, 953, Rogers Ruhega (Chadema) 26, 303 na Malebo Michael (CUF) 625.
Jimbo la Monduli
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,025, Namelock Sokoine (CCM) 25,925 na Navaya Ndaskoi (ACT Wazalendo) 367.
Jimbo la Kibaha Mjini
Ubunge: Silvestry Koka (CCM) 31,462, Paul Mtally (Chadema) 24,860, Habibu Mchange (ACT Wazalendo) 3,438, Gombati Waziri (CCK) 259, Betha Mpata (APPT), 120 na Kibona Ally (AFP) 108.
Jimbo la Arumeru Mashariki
Ubunge: Joshua Nassari (Chadema) 86, 694, Pallaghyo John (CCM) 31, 847, Batuli Ismail (ACT Wazalendo) na Mgina Ibrahim (AFP) 236.
Jimbo la Serengeti
Ubunge: Marwa Ryoba (Chadema) 40, 059, Dk Stephen Kebwe (CCM) 39, 232, Burito Thomas (ACT Wazalendo) 1, 445, Imakulata Mniko (CUF) 328 na Mosena Nyambabe (NCCR-Mageuzi) 408.
Jimbo la Kahama Mjini
Ubunge: Jumanne Kishimba (CCM) 47,553, James Lembeli (Chadema) 30,122 na Bobson Wambura (ACT Wazalendo) 605.
Jimbo la Babati Mjini
Ubunge: Pauline Gekul (Chadema) 21,970 na Kisyeri Chambiri (CCM) 16,434.
Jimbo la Shinyanga Mjini
Ubunge: Steven Masele (CCM) 35,858, Patrobas Katambi (Chadema) 31,027, Nyangaki Shilungushela (ACT Wazalendo) 411 na Emiliana Tambwe (APPT) 178.
Jimbo la Moshi Mjini
Ubunge: Jaffar Michael (Chadema) 51,646, Davis Mosha(CCM) 26,920, Buni Ramole (ACT-Wazalendo) 634, Issack Kireti (Sau) 181 na Godlisen Kitali (UDP) 35.
Jimbo la Dodoma Mjini
Ubunge: Antony Mavunde (CCM) 84,512, Benson Kigaila (Chadema), 42, 140 na Christina Alex (ACT Wazalendo) 927.
Jimbo la Njombe Kaskazini
Ubunge: Joram Hongoli (CCM) 20, 430 na Edwin Swale (Chadema) 10, 407.
Jimbo la Kondoa Mjini
Ubunge: Edwin Sanda (CCM) 13, 333, Ally Kambi (CUF) 6,783, Misanya Ally (Chadema) 1,822, Maulid Majala (ACT Wazalendo) na Salimu Rashidi (UDP) 53.
Jimbo la Bukombe
Ubunge: Dotto Biteko (CCM) 47,147, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) 29,929 na Dick Bagamba (ACT Wazalendo) 1,673.
Jimbo la Bunda Mjini
Ubunge: Ester Bulaya (Chadema) 28, 508, Stephen Wasira (CCM) 19, 126 na Maganya Kulwa (ACT Wazalendo) 293.
Jimbo la Tarime Vijijini
Ubunge: John Heche (Chadema) 47,249, Christopher Kangoye (CCM) 42,325, Charles Mwera (ACT Wazalendo) 1,846 na Tingwa Migera (Chausta) 367.
Jimbo la Hai
Ubunge: Freeman Mbowe (Chadema) 51,124, Danstan Mallya (CCM) 26,996, Nuru Mohammed (ACT-Wazalendo) 318 na Ndashuka Issack (APPT-Maendeleo) 279.
Jimbo la Mbogwe
Ubunge: Augustino Masele (CCM) 32,921, Nicodemus Maganga (Chadema) 13,975 na Andrew Mnuke (ACT Wazalendo) 5,464.
Jimbo la Busega
Ubunge: Dk Raphael Chegeni (CCM) 40,977, David William (Chadema) 26,995 na Zangi Robart (UDP) 802.
Jimbo la Msalala
Ubunge: Ezekiel Maige (CCM) 36,010, Paulo Malaika(Chadema) 20, 124, Marco Suwa (ACT Wazalendo) 672 na Abeid Ibeshi (UDP) 251.
Jimbo la Ngara
Ubunge: Alex Gashaza (CCM) 53,387, Dk Bujari Simon (Chadema) 35,254, Helen Gozi (NCCR-Mageuzi) 997 na Dotto Jasson Bahemu (ACT Wazalendo) 440.
Jimbo la Kisarawe
Ubunge: Seleman Jaffo (CCM) 28, 054, Rashid Mwishehe (CUF) 8, 863 na Asha Chuma (UDP) 364.
Jimbo la Bagamoyo
Ubunge: Dk Shukuru Kawambwa (CCM) 26,434, Andrew Kasambala (CUF) 16,330, Mwamini Saidi (UMD) 418 na Saidi Athman (ACT Wazalendo) 418.
Jimbo la Ilemela
Ubunge: Angelina Mabula (CCM) 85,424, Highness Kiwia(Chadema) 61, 679 na Addam Kimwaga (ACT Wazalendo) 3,910.
Jimbo la Bukoba Mjini
Ubunge: Wilfred Lwakatare (Chadema) alipata kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565.
Jimbo la Ilala
Ubunge: Mussa Azzan Zungu wa CCM alishinda kwa kupata kura 35,518 dhidi ya Hassanal Rajabal wa Chadema aliyepata kura 32,333.