Kwa matokeo ya mchezo huo, Liverpool wanapanda kileleni baada ya kufikisha pointi 81, huku Manchester City wenye michezo miwili mkononi wakiwa nafasi ya pili kwa pointi 80.
Majogoo wa jiji walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 18 kipindi cha kwanza kupitia kwa Joe Allen, baadaye dakika ya 53, Daniel Sturridge akifunga bao la pili, huku bao la tatu likifungwa dakika ya 55 kupitia kwa Luis Suarez.
Wakati Liverpool wakiamini watashinda mechi ya leo, kibao kilibadilika dakika ya 79 baada ya Damien Delaney kusawazisha bao la kwanza.
Liverpool wakazidi kuchanganyikiwa na kuona dakika haziendi. Mnamo dakika ya 88 Dwight Gayle aliandika bao la tatu na mechi kuisha kwa sare ya 3-3.
Baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa, Luis Suarez aliangua kilio kikubwa kwa kuamini kuwa kuna asilimia kubwa wameshaweka reheni mbio zao za ubingwa.
Liverpool wamebakiwa na mechi moja mkononi ambayo wakishinda watafikisha pointi 84, wakati Man city wakishinda mechi zao mbili watafikisha pointi 86 na kutwaa taji.
Kama Man City watashinda mechi moja na kufungwa moja, halafu Liverpool wakashinda mechi ya mwisho, basi majogoo hao wa jiji watafanikiwa kutwaa ubingwa.
Liverpool wanategemea muujiza wa soka kutokea.