Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema.
Alitoa ahadi hiyo wakati akiwaweka wakfu viongozi wapya walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mbele ya Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini, Rachel Mashishanga.
Alisema maono aliyoyapata, chama hicho kitakuwa mkombozi kwa Watanzania katika kuwaletea maendeleo na si chama kingine, hivyo atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kinapata ushindi katika majimbo ya Kishapu na Shinyanga Mjini.
“Magari yangu mawili yatatumika kufanya kampeni kwa gharama zangu katika majimbo haya kutokana na kutokuwa na viongozi wazuri na kutozingatia maslahi ya wananchi,” alisema Mombeki.
Aidha, alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoachwa na Mwalimu Julius Nyerere, siyo cha sasa kwani hakina sera nzuri, viongozi wabovu ambao hawafuati sera ya chama hicho na badala yake wanafuata mambo yao binafsi.
CHANZO:
NIPASHE