EACC YAMUA KUWACHUKULIA HATUA WABUNGE WALIOANZISHA VURUGU JUZI KWENYE BUNGE LA KENYA.

By | 04:05

Tume ya Maadili na Kupambana na Rushwa Kenya (EACC) imeanzisha uchunguzi dhidi ya Wabunge walioanzisha vurugu siku ya juzi December 18 katika kikao cha Bunge maalum na kupelekea wabunge kadhaa kujeruhiwa, muda mfupi baadaye Kikao hicho kikaahirishwa.
Mkuu wa Tume hiyo Mumo Matemu, amesema kwa mujibu wa sura ya sita ya katiba kuhusu uongozi na namna ya kujiendesha Wabunge hao walikiuka Sheria hiyo, hivyo tume hiyo imeamua kulitathimini suala hilo na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika vurugu hizo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya pande mbili za Chama Tawala na vyama vya Upinzani kushindwa kuendeleza mjadala uliokuwa ukijadiliwa wa mapendekezo ya Sheria ya Usalama wa Nchi hiyo, kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye masuala ya Usalama.
Newer Post Older Post Home