Barani ulaya kila kitu hutawaliwa na tarakimu ambazo huwakilisha takwimu ambazo
huhifadhiwa ili kuweka kumbukumbu ya jinsi ya kuendesha masuala mbalimbali kuanzia
siasa , uchumi , biashara binafsi za watu na hata kwenye ulimwengu wa michezo .
Kwenye michezo takwimu ambazo zimezoeleka ni zile za kuonyesha jinsi wachezaji
wanavyofanya kazi uwanja kwa maana ya asilia ya juhudi na mahali ambako kocha
na wasaidizi wake wa masuala ya ufundi wanaweza kutambua ubora na udhaifu .
Hivi karibui takwimu zimeitaja klabu ya Manchester City kuwa timu ambayo ina
wastani wa umri mkubwa kuliko klabu zote zinazoshiriki ligi za soka nchini England .
Takwimu hizi zimeonyesha kuwa Manchester City ina wastani wa umri wa miaka
28.8 kwa wachezaji wake umri ambao ni mkubwa kuliko klabu zote kubwa za
ligi tano bora barani ulaya kwa maana ya Epl , Primera Liga , Serie A , Bundesliga
na Ligue 1.
Kwa jumla Man City imeshika nafasi ya 7 katika utafiti uliofanyw akwa kutazama
wastani wa umri wa wachezaji wa klabu zipatazo 500 barani ulaya kuanzia ligi kuu
mpaka madaraja ya chini.
Manchester City ina wachezaji 12 ambao wana umri kuanzia miaka 29 kwenda
mbele wakiwemo Kina Martin Demichelis , Frank Lampard ,Bacary Sagna ,
Yaya Toure , Gael Clichy , Jesus Navas na wengine .
Wachezaji kama Nemanja Vidic wanaifanya Ligi ya Serie A iwe ligi inayoongoza
kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko zote huku ikifuatiwa na Cyrstal Palace
, Stoke City,West Bromwich Albion na QPR .
Kwa upande wa timu ambazo zina wastani wa umri mdogo ni Newcastle United ,
Manchester United , Southampton , Arsenal na Liverpool .