Polisi Mkoani Ruvuma wanafanya uchunguzi wa tukio ambalo mtu mmoja aliuawa kwa kulipukiwa na bomu alilotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa kwenye doria usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana SAIDI MWAMBUNGU amesema katika tukio
hilo polisi wawili pia walijeruhiwa lakini hali zao zinaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mikoa watu wanne waliokuwa na mtu huyo
ambaye hajatambuli w a jina lake walikimbia lakini polisi wa l ika ma
ta simu za watu hao na mtu huyo aliyeuawa na bomu.
Hilo ni tukio la tatu mkoani Ruvuma kwa polisi kurushiwa mabomu na
raia na Mkurugenzi wa Mak o sa ya Jinai nchini Bwana ISAYA MUNGULU
alikuwa anatarajia kuwasili Songea leo kufuatilia tukio hilo.