MISS WORLD YAFUTA KIPENGELE CHA VAZI LA UFUKWENI.

By | 09:24

               miss worldd
Waandaaji wa mashindano ya urembo ya dunia maarufu kama Miss World wamefuta sehemu ya shindano hilo inayohusisha warembo wakiwa wamevalia nguo za kuogelea maarufu kama vazi la ufukweni au Beach Wear.

Mkurugenzi wa mashindano haya Chris Wilmer amesema kuwa sababu ya kufutwa kwa kipengele cha mashindano ya cha nguo ya kuogelea ni kushindwa kuendana na vipengele vingine vya mashindano haya .
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mashindano haya pamoja na kuwa mashindano ya urembo lakini hayahusishi urembo pekee bali urembo na sababu maalum na hakukuwa na sababu yoyote maalum ya kujumuisha kipengele cha nguo za kuogelea .
                   Miss World imeamua kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.
Miss World imeamua kufuta kipengele cha vazi la ufukweni.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Mshindi wa Miss World anapaswa kuwa balozi na msemaji wa jamii ya watu sio malkia wa urembo pekee .
Maadili na kile anachowakilisha mshindi wa Miss World ndio kinachotazamwa kwa mshindi hivyo kwa sababu hiyo Miss World haitakuwa na kipengele cha shindano la nguo ya kuogelea .
Newer Post Older Post Home