Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Wema Sepetu. BAADA ya kudaiwa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa alichoropoa mimba zake mbili, mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’ ameibuka na kujibu mapigo kwamba mwanamuziki huyo hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, Risasi Jumamosi linakupa mchapo kamili. CHANZO CHA YOTE Akizungumza na GlobalTV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu. “Sikukaa sana akaniletea maneno…oooh mara hivi mara vile…eti imetoka.
Nikasema poa, labda haikuwa riziki. Nikampa ya pili, nayo pia akatoa. Nikasema bora niachane naye na huo ndiyo ukawa mwisho wa mimi na Penny.” KILICHOFUATA Baada ya habari hiyo kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Amani wiki iliyopita, Penny alijibu mapigo na kudai kwamba ni kweli staa huyo alikuwa akimridhisha kimapenzi lakini hakuwa na uwezo wa kumpachika mimba kama alivyodai.“Diamond ni mwanaume kama wanaume wengine lakini hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, muulizeni vizuri tatizo ni nini,” alisema Penny.