Mwanamke anapokuwa mjamzito hasa
unapofika wakati wa kukaribia kujifungua huwa makini sana ili aweze
kujifungua salama, lakini kuna wakati ambao hujikuta ana changamoto
kutokana na mazingira ambayo uchungu wa kujifungua unampata.
Hii inasikitisha kutokana na kitendo cha
mama mmoja kujikuta akilazimika kujifungua katika eneo la parking ya
magari nje ya Club kutokana na kupata uchungu akiwa kwenye taxi
iliyokuwa ikimpeleka hospitali Tennessee, Marekani.
Maafisa wa zimamoto walipofika eneo la
tukio walimkuta mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 akiwa tayari
amejifungua na amempakata mtoto wake ndani ya taxi hiyo.
Baadaye mama na mtoto wake walipelekwa Hospitali ya St. Thomas Midtown.
Meneja wa Club ambayo mtoto huyo
alizaliwa kwenye eneo la parking amesema wana mpango wa kumpa zawadi
mwanamke huyo pamoja na mtoto wake kiasi cha dola 500 pamoja na zawadi
nyingine mbalimbali pamoja na toy za kuchezea.