raheem Sterling
Mshambuliaji
kinda wa Liverpool, Raheem Sterling amekabidhiwa Tuzo ya Mwanasoka bora
chipukizi mwaka 2014 na Chama cha soka cha England FA.
Sterling alikabidhiwa tuzo hiyo kabla ya Mechi wa ligi kuu ya England kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal wakiwa uwanja wa nyumbani Anfield, ambapo mechi hiyo imemalizika kwa sare ya goli 2-2.
FA imekuwa na utaratibu wa kutoa tuzo ya Mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji chipukizi wanaofanya vizuri katika mchezo wa soka.