Umoja wa mataifa unasema kuwa Sudan imewafukuza maafisa wake wawili wakuu kutoka nchini humo.
Katibu
mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, amelishutumu taifa hilo kwa
kumfurusha mshirikishi mkuu wa utoaji msaada Ali Al-Zatari, na
mkurugenzi mkuu wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa mataifa Nchini humo
Yvonne Helle.Haijafahamika ni kwa nini wawili hao wamefurushwa.
Uhusiano kati ya Umoja wa mataifa na serikali ya Sudan umekuwa m'baya tangu walinda amani wa umoja wa Afrika kuchunguza ripoti ya ubakaji ulioendeshwa na wanajeshi wa taifa hilo katika eneo la Darfur mwezi uliopita.