Tatizo la vifo vya wanawake
wajawazito na watoto limeanza kupungua wilayani Monduli mkoani Arusha
ikiwa ni matokeo ya wananchi kujitolea kuchangia ujenzi wa zahanati na
vituo vya afya na pia kuhamasika kupokea ushauri wa wataalam wa afya
ukiwemo wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa moja ya zahanati zilizojengwa
na wanachi katika kijiji cha NAFCO kaya ya loksale mganga mkuu wa
wilaya ya monduli Dr.Zaveri Peter Benela amesema pamoja na changamoto
zilizopo ikiwemo ya mila potofu asilimia kubwa ya wannachi
wanaendelea kubadilika.
Mtendaji wa kata ya lokisale Bw.Ahmed Mhando amesema kukamilika
kwa zahanati ya kijiji cha NAFCO iliyoghaimu zaidi ya milioni 39
pamoja na kuwapunguzia wananchi umbali wa kuzifikia huduma za afya
umewaongezea hamasa ya kujiunga na huduma ya mfuko wa afya yajamiI.
Akizungumzia hatua hiyo baada ya kuzindua na kutembelea zahanati
hiyo waziri mkuu aliyejiuzulu Mh.Edwad Lowasa amewataka watendaji
kuongeza uhamasishaji wa wananchi kujiunga na huduma ya mfuko wa afya
ya jamii.
Mh Lowasa ambaye pia ni mbunge wa Monduli amesema mfuko wa afya ya
jamii ndio njia pekee ya kuwawezesha wananchi kupata tiba wakati wote
na kwa gharama nafuu na kwamba licha ya kuwepo kwa changamoto
zinaendele kufanyiwa kazi.