Kikao
cha Bunge la Kenya kilisimama kwa takribani dakika 30 kutokana na
kutofautiana kwa Wabunge hao kuhusiana na msimamo wao kutofautiana
wakati wakiendelea na mjadala unaohusu mabadiliko ya Sheria ya Usalama
wa Nchi hiyo kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye
masuala ya Usalama.
Wabunge wa upinzani walipinga muswada
huo kwa kutupa karatasi chini, Bunge likaahirishwa ambapo hali ya hewa
ilikuwa mbaya na baadaye Wabunge hao kupigana, wengine wakichaniana nguo
na hata kuumizana.
Wabunge wa Upinzani waligomea muswada huo na kuanza kuimba, Bunge hilo likasitishwa.