Mbunge wa Zitto Kabwe
leo amewahutubia Wananchi wa Mtwara kupitia mkutano ulioitishwa na
chama cha Wananchi CUF na kutoa ufafanuzi juu ya sakata la account ya
Tegeta Escrow.
Akizungumzia sakata hilo Zitto Kabwe
amesema kuwa baadhi ya viongozi waliohusika na sakata hilo ambao mpaka
hivi sasa hawajachukuliwa hatua yoyote lazima wachukuliwe kwa kuwa
serikali haiwezi kupingana na maazimio ya bunge.
Sisi
lazima tuutumie mwaka 2015 kama mwaka wa uwajibishaji, mwaka wa
kuwajibishana… safari hii mmewawajibisha kwenye Seikali za Mitaa,
hongereni sana, tunaenda kuwawajibisha kwenye Serikali kuu sasa…”– Zitto Kabwe.