Iliwahi kusikika Hekaheka inayofanana na hii ya leo yani mganga amedai anaweza kurudisha watu waliofariki.. ya leo ni kwamba mama mmoja wa Mabwepande, alifiwa na mtoto wake katika mazingira ya kutatanisha.. akakutana na mama mmoja ambaye alimwambia kuwa binti yake atakuwa amefariki kifo cha kishirikina, akamkutanisha na mama ambae aliwahi kurudishiwa mtoto wake.
Mama huyo amesema walianza mawasiliano,
mganga huyo akamwambia atoe sh 100.. baadae walienda kwa mganga huyo
Dodoma na kuoneshwa binti ambae aliona kama ni binti yake, mganga
akataka allipwe sh. milioni mbili na shilingi 100 ili aweze kumrudisha.
Walipofika Dar hawakumuona mtoto kwenye
gari, wakampigia simu mganga akawaambia waendelee kusubiri, baadae
wakagundua kuwa jamaa hakuwa mganga ila ni tapeli.