Manchester United ilipokwaana na Derby
Timu ya Manchester United watakwenda nchini Marekani kujiwinda na msimu ujao baada ya msimu huu kumalizika.
Wakiwa
katika maandalizi hayo Man United, ,watacheza na Barcelona katika dimba
la Levi's Mjini Santa Clara, California, hapo Julai 25.Mechi nyingine za Man United huko Chicago ni Julai 29 dhidi ya Paris St Germain na kisha dhidi ya Klabu ya Mexico, Club America, watakayocheza Mjini Seattle na ile ya Klabu ya Marekani, San Jose Earthquakes.
Mechi hizi ni za Mashindano ya International Champions Cup ambayo Mwaka Jana, Man United iliitwanga Liverpool 3-1 kwenye Fainali na kubeba Kombe.