Ligi kuu ya England inakaribia ukingoni, na tayari timu mbalimbali zimeshapata taswira kamili ya nini zimepanda kwa msimu mzima wa ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubw a ndani yake.
Chelsea bado ina matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na wiki ijayo inaweza kutangaza ubingwa endapo itaifunga Crystal Palace baada ya jana kutoka sare ya 0-0 na Arsenal na hadi sasa ndiyo inayoongoza kwenye msimo wa ligi ikiwa na pointi zake 77.
Stori ambayo ipo kwenye headlines kwa sasa ni kuhusu kiungo wa Chalsea Eden Hazard ambaye amechagulia kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha wachezaji wa kulipwa England PFA
Mchezaji huyo nyota raia wa Ubelgiji
ameifungia Chelsea mabao 18 akiiwezesha kutwaa taji la kombe la ligi
maarufu Capital One na kuisaida kwa sasa kusaka ubingwa kwa mara
nyingine tangu mwaka 2010.
Hazard amekabidhiwa zawadi iyo katika hotel ya Grosvenor Hotel iliyopo London ikiwa ni kutokana na kuonyesha kiwango kizuri akiwa ndani ya kikosi hicho kwa kiasi kikubwa.
Tuzo ya heshima ilikwenda na Steven Gerrard na Frank Lampard kutokana na mchango wao mkubwa kwenye ligi kuu ya England
Related Items