Hii ishu inahusiana na tukio ambalo
liliripotiwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo Magazeti kuiandika sana..
ilishtua wengi, hata mimi iinishtua pia.. marehemu amefariki, ndugu
wamefanya mazishi.. siku chache baadae wakaja watu wasiofahamika
wakafukua kaburi na kuiba nguo mabegi mawili ambazo alizikwa nazo
marehemu.
Hizi ni picha ambazo nimekusogezea hapa.. ndugu waliamua kulijenga upya baada ya wezi hao kubomoa na kuiba vilivyokuwemo ndani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani
limethibitisha tukio hilo, wanawatafuta waliovunja kaburi hilo na
kufanya uhalifu wa kuiba nguo na vitu vingine alivyozikwa navyo.
Shuhuda mmoja amesema walikuta kaburi
limechimbuliwa, nguo zimetolewa na nyingine walikuta zimetupwa vichakani
ikabidi wazichome moto.
Related Items