Kampuni
ya Tesla Motors, inayounda betri ya gari, imetangaza kuwa, ina mpango
wa kuuza teknolojia ya betri yenye uwezo wa kuzalisha kawi ya matumizi
majumbani na kwenye biashara mbalimbali.
Bilionea muasisi wa
Tesla, Elon Musk, anasema kuwa betri hiyo mpya itawezesha watu wengi
kupata afueni kutokana na kuwa na uhakika wa nguvu za umeme bila ya
kukatizwa.Anasema kuwa teknolojia hiyo mpya itabadilisha mtizamo wa watu Duniani wa namna ya kutumia kawi.
Tesla tayari inatengeneza betri zinazotumiwa na magari ya umeme yasotumia petrol.
Betri hizo, aina ya lithium-ion, huchajiwa mara-kwa-mara. Kwa teknolijia hiohio betri za kutumia majumbani na katika biashara zinatengenezwa.
Inakisiwa, Tesla itachuma $4.5bn kwa mauzo hayo. Lakini wadadisi wanadhani huenda Tesla ukakumbwa na ushindani mkubwa na makampuni mengine yenye masilahi hayo, kama General Elecctric na LG ya Korea Kusini.
BBC SWAHILI.