Leo Tanzania imeungana na Mataifa mengine duniani kuadhimisha
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyanyakazi Duniani Maarufu kwa jina la Mei
Mosi ambayo Kitaifa hapa nchini yamefanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba
Ilelema Mkoani Mwanza. Maadhimisho hayo yamekuwa na Mvuto wa pekee
kutokana na ambavyo wananchi na wafanyakazi kutoka Sekta mbalimbali za
Serikali na binafsi walivyojitokeza kushiriki na kujionea maadhimisho
hayo katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Mgeni Rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambapo Kauli mbiu mwaka huu katika Maadhimisho
hayo ilikuwa ni "Mfanyakazi Jiandikishe, Kura Yako Ina Thamani katika
Maendeleo Yetu"
Katika Picha Juu ni Maandamano ya Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza
yakitoka katika Uwanja wa Furahisha yalipokuwa Mabanda ya Maonyesho ya
Siku hii ya Mei Mosi yakielekea katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo
katika ujumbe wa Muungano huo ulikuwa ni Kuwezeshwa Mitaji kwa ajili ya
kuinua shughuli zao za Biashara, Kuendelea kutengewa Maeneo kwa ajili ya
shughuli zao.
Na:George GB Pazzo
Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza.
Maandamano ya Wafanyakazi mbalimbali yakielekea katika Uwanja wa CCM Kirumba
Wafanyakazi wa Bank ya Posta wakiingia katika Uwanja wa CCM kirumba
Wanachama wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza wakiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba
Altaf Mansoor ambae ni Mlezi wa Timu ya Watoto wa Mitaani Mkoani Mwanza
ambayo ilichukua Kombe la Dunia kwa Watoto wanaoishi Mitaa Mwana jana
akiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba hii leo huku akiwa ameshikilia
Kombe la Timu hiyo.
Altaf Mansoor kutoka Kampuni ya Mafuta ya MOIL ambae ni Mlezi wa Timu ya
Watoto wa Mitaani Mkoani Mwanza ambayo ilichukua Kombe la Dunia kwa
Watoto wanaoishi Mitaa Mwana jana akiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba
hii leo huku akiwa ameshikilia Kombe la Timu hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL wakiingia katika Uwanja wa CCM Kirumba
Taswira ya Uwanja ilivyokuwa
StarTimes Tanzania pia walikuwepo katika Maadhimisho hayo.
BINAGI MEDIA GROUP SOURCE.
Related Items