Mke wa mrithi wa ufalme wa Uingereza Prince William amejifungua mtoto wa kike.
Habari
iliyotumwa kupitia kwa mtandao wa Twitter kutoka kwa ikulu ya
Kensington ilisema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa salama kabla ya saa
mbili unusu saa za uingereza.Mtoto huyo aliye na uzito wa kilo tatu nukta saba alizaliwa muda mfupi baada ya kuwasili kweny hospitali moja mjini London.