SERIKALI YA IVORY COAST IMEKUJA NA SHERIA HII KWA WANAWAKE WANAOPENDA UREMBO.

By | 04:54
                 http://i2.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/05/hili.jpg
Wanawake wengi duniani wanaamini moja ya vitu vinavyowaongezea mvuto wa ngozi zao ni kutumia mafuta yanayobadilisha ngozi zao au kwa jina lingine mafuta ya kujichubua ngozi.
Wengi wamekuwa wakifanya hivyo na kukumbana na maradhi mengi ikiwemo kupata kansa ya ngozi kwa sababu kitaalamu wanatumia kemikali ambazo ni kali na hazifai kwa matumizi ya ngozi ya binadamu.
Ivory Coast imeingia kwenye Headlines baada ya Wizara ya afya ya nchini humo kupiga marufuku uingizwaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa zozote zenye uwezo wa kuchubua rangi ya ngozi ya binadamu .
Bidhaa nyingi za kijichubua rangi ya ngozi zinauzwa katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika na sasa Serikali imeweka sheria kali ya matumizi ya kemikali hizo ambazo kwa miaka ya sasa hata wanaume wamekuwa wakitumia na kufanya idadi kuwa kubwa.
Christian Doudouko ambaye ni Afisa anayesimamia matumizi ya madawa nchini humo amesema wanawake wengi wamekuwa wakipatwa na magonjwa ya ngozi yanayopelekea saratani bila kujijua.
Newer Post Older Post Home