Kuna ishu ya jinsia ya mtoto anaezaliwa,
kati ya wazazi huenda ikatokea kati yao akawepo mmoja ambae anatamani
kuwa na mtoto wa kike na mwingine akawa anatamani awe na mtoto wa
kiume..
Rameshwar Rao
aliamua kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka
mitatu kisa tu mwanamke huyo amejifungua mtoto wa kike wakati mwanaume
alikuwa anahitaji kuwa na mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka kugundua
ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka aitoe
mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa kuitoa na
kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Mwanamke huyo alitaka kukimbia baada ya
kujifungua, mwanaume akaamua kumkamata na kumfungia kwenye choo pamoja
na mtoto wao wa kike kwa muda wa miaka mitatu huku akiwa anawapa wali na
maji kwenye bakuli kila siku.
Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na
polisi baada ya marafiki wa familia yake kugundua kitendo alichokifanya
kwa mkewe lakini mke wake amewaomba polisi hao kumwachia huru ili
waendelee kuishi pamoja.