Unapozungumzia ubora wa mchezaji si wengi wanaweza
kubishana na ukweli kwamba Andres Iniesta ni moja kati
ya viungo bora kwneye soka la kimataifa na ameweza
kubakia katika ubora na kiwango cha juu kwa muda
mrefu bila kushuka.
Kiungo huyu amekuwa sehemu ya mafasikio ya klabu
hii ya Kihispania kwa muda mrefu tangu alipoanza kucheza
akiwa amepandishwa toka kwenye timu za vijana za klabu
hii ambayo imekuwa ikisifika kwa kuamini na kutengeneza
vijana wake yenyewe.
Iniesta ametwaa mataji yote yaliyoko kwenye soka la ushindani
kuanzia ligi ya Hispania , Kombe la Mfalme , Super Coppa Espana,
European Super Cup , kombe la dunia kwa vilabu , Kombe la dunia
la FIFA pamoja na michuano ya kombe la mataifa ya ulaya .
Kiungo
Andres Iniesta ndio mchezaji pekee ambaye
amewahi kutwaa tuzo ya
mchezaji bora wa mechi
kwenye fainali za mashindano makubwa matatu
tofauti.
soka la Hispania Iniesta ameweza kudumu wakati
wachezaji wengi wamekuja na kupita na cha kushanga
za ni jinsi ambavyo ameendelea kuwa bora .
Jumamosi ya wiki hii iliyopita , Andres Iniesta aliweka
rekodi ya kuwa mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa
tuzo ya mchezaji bora wa mechi yaani Man Of The Match
kwenye fainali za Ligi ya mabingwa , kombe la Ulaya na kombe
la dunia baada ya kutwaa tuzo ya Man Of The Match kwenye
fainali dhidi ya Juventus .
Iniesta anakuwa mchezaji pekee ambaye amewahi kuweka rekodi
hiyo akiwa katika ubora wake ule ule ambao amezoeleka kuwa nao .
Iniesta alikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa Barcelona
dhidi ya Juventus baada ya kutoa pasi ya mwisho iliyosaidia bao la
kwanza lililofungwa na Ivan Rakitic kwenye dakika ya 4 na kwenye
mchezo wote akiwa kama nahodha kabla ya kutolewa na nafasi yake
kuchukuliwa na Xavi Hernandez.
Related Items