wakihofia kuzipata hivi karibuni hatimaye zimekuwa kweli baada
ya kipa namba moja wa klabu hiyo Mhispania David De Gea
kuiambia klabu hiyo kuwa anataka kuhamia Real Madrid .
De Gea kupitia wakala wake ameiarifu United kuwa dhamira
yake ni kujiunga na Madrid na amefikia uamuzi huo baada ya
kipindi kirefu cha kuwaza na kuamua ni hatua ipi bora ya kufuata
kwenye mustakabali wake .
De Gea amekaa na United kwa muda wa miaka minne tangu
aliposajiliwa toka Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho
ambayo iliweka rekodi kwa makipa ya paundi milioni 17
na amekaa United kwa muda wa miaka minne ,
muda ambao amepia hatua kubwa kiasi cha kufikia
kuwa na kiwango cha ubora wa dunia .
Hivi karibuni De Gea alipewa ofa ya kuongezewa
mshahara mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ofa ambayo
hajaikubali akiwa amefikia uamuzi wa kurudi nyumbani kwao
kwenye mji aliozaliwa na kukulia huku akipata fursa ya kuwa
karibu na mpenzi wake Edurne .
De Gea amekuwa kwenye mipango ya Real Madrid kwa muda
mrefu ambapo klabu hiyo imemuweka kama chaguo namba moja
la kuziba nafasi ya mkongwe Iker Casillas ambaye umri wake
unazidi kuwa mkubwa .
Endapo usajili huu wa David De Gea kuondoka United na kuhamia
Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu , kipa huyo atakuwa
mchezaji wa tano kuondoka United baada ya Cristiano Ronaldo ,
David Beckham , Ruud Van Nistelrooy na Gabriel Heinze.