Story nyingine ni kama utani hivi ukivuta picha.. eti mteja kaja na Milioni 200TSHS zote ni sarafu na anataka huduma yako kabisa !!
Story iko kwenye headlines toka Shenyang,
China… mteja kaingia showroom ambako wanauza magari na cash yake
mkononi, amejikusanyia dola 106,000 ambazo ni sawa na Mil. 232, ishu ni
kwamba hela zote ni sarafu, bora hata ingekuwa noti yani.
Jukumu lingine limewakuta wafanyakazi wa
showroom hiyo ambao walilazimika kuanza kushusha hela hizo kutoka
kwenye gari lililokuwa limebeba mzigo huo ambao ulizidi uzito wa tani
nne. 
Mr. Gan
ndio mteja mwenyewe aliyekuja na mzigo huo, amesema yeye anauza mafuta
kwenye sheli.. kwa hiyo chenji hizo amezikusanya hapohapo akaona
ajinunulie gari ya kutembelea !!
Yani jamaa alichokiona amerahisisha ni kufunga hela hizo kwenye vibunda vidogovidogo.
Huyu mteja akija kwako unamsaidiaje mtu wangu?
Related Items