Klabu ya Liverpool leo hii imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo James Milner kutoka Manchester City.
Milner mwenye umri wa miaka 29, alipiga chini nafasi ya kuendelea kubaki Etihad Stadium ili awese kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza chini ya Brendan Rogers msimu ujao.
Milner amemaliza mkataba wake na City, na atajiunga rasmi na Liverpool tarehe 1 mwezi ujao.
Mchezaji huyo alijiunga na City akitokea Aston Villa miaka minne iliyopita na amefanikiwa kutwaa makombe mawili ya Ligi kuu ya Uingereza pamoja na FA Cup.