MAREKANI:TAZAMA UBAGUZI ULIOTOKEA NDANI YA NDEGE.

By | 12:25

0 
Neno ubaguzi ni kama lilianza kusahaulika hivi duniani.. lakini kwa sasa linasikika karibu kila siku, matukio ya watu wenye asili ya Afrika kupigwa risasi Marekani yalichukua headlines kubwa sana na bado hayajasahaulika !!
Hiki kilichofanywa na mhudumu wa kwenye ndege ya Shirika la ndege la United Airlines, nacho kimelalamikiwa na kuhusishwa na ishu ya ubaguzi.. mhudumu huyo aligoma kumpatia abiria mmoja mwanamke, Tahera Ahmed soda ya kopo, alichomjibu ni kwamba eti hawezi kumpa kwa sababu anaweza kutumia kopo hilo la soda kama silaha ndani ya ndege.
Coke 
Mabosi wa Shirika hilo hawajaicha hii ishu hivihivi.. mhudumu huyo amesimamishwa kazi.
Kitu kilichomkasirisha zaidi Tahera ni ishu ya yeye kukataliwa soda ya kopo alafu jirani yake akapewa bia ya kopo.. mwanamke huyo akalalamika kwamba labda kwa vile yeye ana asili ya Kiarabu ndio maana akakataliwa !!
Hapa kuna video inayoonesha mwanamke huyo akielezea ilivyokuwa

Flight US
Hii ilikuwa post ya Tahera kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya kutokea kwa ishu hiyo.
Newer Post Older Post Home