Wanachama wa kundi la Hamas
Mahakama nchini Misri imefuta hukumu ya awali ambayo ilikitaja chama cha Hamas cha Palestina kama kikundi cha kigaidi.
Imefuta hukumu hiyo kwa sababu mahakama iliyotoa hukumu hiyo haikuwa na uhalali wa kufanya hivyo.Misri inaonekana kama ni msuluhishi mwenye nguvu kwenye mzozo kati ya Israel na Hamas, ambayo inatawala eneo la ukanda wa Gaza.
Lakini tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohamed Morsi ,uhusiano baina ya Misri na Hamas umedondoka.
Hamas ilikuwa ni chama dada cha Muslim Brotherhood ambacho ni chama cha rais Morsi.
Na sasa Muslim Brotherhood imepigwa marufuku nchini Misri.