Mwanariadha Mo Farah wa Uingereza
amekasirishwa na hatua ya kulitia jina lake katika matope na sasa
anataka majibu kufuatia madai yanayomuhusisha kocha wake Alberto Salazar
na dawa za kusisimua misuli.
Bingwa huyo wa Olimpiki kutoka
Uingereza na vilevile bingwa wa dunia amesema kuwa atakuwa mtu wa kwanza
kumuacha Salazar iwapo madai yaliotolewa na BBC ni ya kweli.Chama cha riadha Uingereza hakina wasiwasi kwa wawili hao kufanya kazi pamoja.
Hakuna madai kwamba Farah amekiuka sheria na kwamba Salazar amekana madai yoyote ya kuhusika na dawa za kusisimua misuli.