Shirika la ujasusi la FBI nchini Marekani linachunguza ni kwa namna gani wadukuzi wa komputa waliweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .
Ofisi ya utumishi ya nchini hiyo inasema karibu watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.