Wadhamini wakuu wa FIFA wameafiki
tangazo la Bwana Blatter kujiuzulu, wakisema kuwa ni hatua bora kuelekea
mageuzi ya shirikisho hilo.
Kampuni ya Coca-Cola inasema inaamini
kuwa uamuzi huo utaisaidia FIFA kuchukua hatua za dharura kushughulikia
masuala yaliyoibuka .Wakuu wa soka barani Ulaya pia wameridhishwa na uamuzi huo.
Wakati huo huo Mwanamfalme wa Jordan Ali bin al Hussein aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais wa FIFA wiki iliyopita ameashiria kuwa anaweza kujiandaa tena kuwania nafasi hiyo.