DR AMOS ADAM WA FIFA KUCHUNGUZWA.

By | 09:33


Image copyrightAFP
Image captionFIFA
Aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya Shirikisho la Soka ulimwenguni FIFA kutoka Nigeria Dr Amos Adam yupo chini ya uchunguzi na kamati ya maadili ya FIFA kutokana na taarifa iliyotolewa hapo jana. Adam alivunja sheria za Fifa lakini Fifa haikuweza kutoa taarifa zaidi kuhusiana na taarifa hiyo.
Alikuwa mjumbe wa kamati kuu kwa muda wa miaka minne hadi mwaka 2010 alipozuiwa kushiriki katika masuala yote yanayohusiana na soka kwa muda wa miaka mitatu lifungiwa kutoka na tuhuma za kuomba fedha ili kupiga kura za uandaaji wa michuano ya kombe la dunia. Alikuwa kiongozi wa juu katika serikali ya Nigeria kwa miaka 20,na alikuwa akifikiriwa kuwa kati ya watu ambao wangemrithi Issa Hayatou katika shirikisho la soka barani afrika (CAF).
Amepigwa faini ya faranga paundi 6341 za kiingereza,adhabu hiyo imetolewa na kamati kuu ya maadili ya Fifa baada ya kupatikana na kosa la kuvunja sheria zinazohusiana na maswala ya rushwa.
Newer Post Older Post Home