EVERTON DHIDI YA MANCHESTER UNITED

By | 11:23


Ripoti za moja kwa moja za mechi za ligi kuu nchini UingerezaJumamosi
18.55pm:Matokeo kamili.
Tottenham 0 - 0 Liverpool FT
Chelsea 2 - 0 Aston Villa FT
Crystal Palace 1 - 3 West Ham L
Everton 0 - 3 Man Utd FT
Man City 5 - 1 Bournemouth FT
Southampton 2 - 2 Leicester L
West Brom 1 - 0 Sunderland FT
18.50pm:Na mechi inakamilika hapa ikiwa Everton wamecharazwa mabao 3 kwa bila na klabu ya Manchester United.Manchester sasa wamelipaza kisasi kibano waliochapa katika msimu wa nyuma
Image copyrightGetty
Image captionFellaini
18.39pm:,Manchester United. Marouane Fellaini anachukua mahala pake Ander Herrera ambaye ametoka
18.25pm:Wayne Rooooney, Jagielka anaokoa hapa.ilikuwa ni hatari sana ikiwa ni dakika ya 24 katika kipindi cha pili.Everton 0 Manchester united 3
18.19pm:Goooooooal Manchester United wapata bao lao la tatu kunako dakika ya 64 kupitia nyota wake Wayne Rooney baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Ander Herrera.
18.00pm:Kipindi cha pili kinaanza kati ya mechi ya Everton dhidi ya Manchester United
17.52pm:Matokeo kufikia wakati wa mapumziko
Tottenham 0 - 0 Liverpool
Chelsea 1 - 0 Aston Villa
Crystal Palace 1 - 1 West Ham
Everton 0 - 2 Man Utd
Image captionSterling afunga bao tatu pekee
Man City 4 - 1 Bournemouth
Southampton 2 - 0 Leicester
West Brom 0 - 0 Sunderland
17.36pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kinakamilika hapa baada ya Everton kukosa bao la wazi .
17.34pm:Manchester united wanacheza gusa ni guse hapa huku Everton wakionekana kurudi nyuma hapa.
Ni kitendo cha kushangaza maana wanafanya kama ambaye wao ndio walio juu.
17.32pm:Romelu Lukaku akosa kichwa kizuri pale baada ya krosi nzuri kutoka kwa Seamus Coleman.
Image copyrightGetty
Image captionwayne Rooney
17.28pm:Matokeo kufikia sasa
Tottenham 0 - 0 liverpool FT
Chelsea 1 - 0 Aston Villa L
Crystal Palace 1 - 1 West Ham L
Everton 0 - 2 Man Utd L
Man City 4 - 1 Bournemouth L
Southampton 1 - 0 Leicester L
West Brom 0 - 0 Sunderland L
17.26pm:Dakika ya 26 Manchester United 2 Everton 0
Image copyrightGetty
Image captionHerrera
17.21pm:Gooooooal Manchester United wapata bao la pili hapa dhidi ya Everton kupitia Anders Herrera.baada ya krossi maridadi iliopigwa na Rojo.
17.19pm: Wachezaji wa Manchester United
01 De Gea 36 Darmian 04 Jones 12 Smalling 05 Rojo 28 Schneiderlin 31 Schweinsteiger 08 Mata 21 Herrera 09 Martial 10 Rooney
17.15pm:Gooooooooooal Manchester United inapata bao la kwanza hapa dhidi ya Everton kunako dakika ya 18 Schneiderlin aifungia manchester United.
Wachezaji wa Everton
24 Howard 23 Coleman 05 Stones 06 Jagielka 32 Galloway 16 McCarthy 18 Barry 12 Lennon 20 Barkley 14 Naismith 10 Lukaku
17.12pm:Manchester City 2 Bournemouth 0
17.10pm:Wayne Rooney anapata nafasi lakini anapiga vibaya,kwakweli nafasi kama hizo hazitokei na Rooney amefanya vibaya sana kwa mchezaji wa kiwango chake.
Image copyrightPA
Image captionLukaku
17.07pm:Wanafanaya masihara hawa mabeki wa Manchester United na kumuachia Lukaku !angepumua kidogo tu wangekuwa kifua mbele hawa Everton
17.06pm:Martial anatoka pale katika lango la Everton lakini Jagielka anamkaba.
17.05pm:Vijana wa Manchester United wanaanza kwa kasi hapa dhidi ya Everton,lakini kumbuka kwamba Everton ni timu ya kuotea mbali ikijiringia mchezaji kama vile Lukaku.
Image copyrightAP
Image captionEverton dhidi ya manchester United
17.00pm:EVERTON DHIDI YA MANCHESTER UNITED.
16.36pm:Na mechi inakamilika hapa Ikiwa Tottenham 0 Liverpool 0.
16.29pm:Lamela atoka Townsend aingia upande wa Liverpool Ibe aingia mahala pake Coutinho
16.25pm: Dakika ya 85 Tottenham 1 Liverpool 0.
16.26pm:Tottenham wafanya shambulizi kupitia Harry Kane lakini mpira uantoka nje do.
Image captionCristian Ericksen
16.13pm: Mpira umesimama huku beki wa pande wa kulia wa Tottenhma Kyle akipata matibabu.
16.10pm:Liverpool inacheza vyema lakini hakuna matokeo yoyote kufikia sasa ikiwa dakika ya sabini katika kipindi cha pili.Adam lalana anatamba na mpira huku na kule lakini hawezi kutoa krosi wala kupiga mkwaju,amekabwa.
16.09PM: Siku nyingi sana Dembele amekuwa akicheza vizuri lakini hii leo amejiimarisha zaidi na kuwa mchezaji anayejituma zaidi miongoni mwa wachezaji wa Tottenham.
16.07pm:Liverpool inaonyesha mchezo mzuri lakini mechi hii ni nguvu mtu,na makabiliano yanaendelea.Erik Lamela ndio mchezaji wa hivi punde kuonywa na refa Craig Pawson baada ya kumuumiza Alberto Moreno.
Image captionJames Milner amlalamikia refa
14.50pm:Timu zote zaonyesha mchezo wa hali ya juu hapa.
Upande wa Liverpool wanaoonekana wakifanya mashambulizi ni Divock Origi,Adam Lalana na Coutinho huku Upande wa Tottenhma safu ya mashambulizi inaongozwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane nad Cristina Ericksen.
14.47pm:Liverpool yaanza kwa kasi kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza cha mechi.
15.45pm:Kipindi cha pili cha mechi katika ya Tottenham dhidi ya Liverpool kimeanza
Image captionLiverpool/Tottenham
15.30pm:Na kipindi cha kwanza kinakamilika ikiwa Tottenham 0 Liverpool 0
15.28pm:Divock Origi na Coutinho waonekana wakishirikiana vizuri hapa lakini bado hawajampatia bao Jurgen Klop,kocha mpya wa Liverpool.
Image captionJurgen Klopp
15.25pm:Tottenham imeonekana kuimarika zaidi na liverpool huku mda wa mapumziko ukiwadia.
15.20pm:Wachezaji wa Tottenham wafanya mashambulizi makali,lakini mambo hayajakuwa mazuri hapa.
Image captionAdam Lalana ashambulia Tottenham
14.56pm:Timu zote zinajitahidi hapa ikiwa kila upande inatafuta kuona lango la mwengine.
Liverpool ilianza kwa kulishambulia lango la Tottenham kwa kasi lakini sasa Tottenham imeanza kulishambulia lango la Liverpool kupitia Harry Kane hapa.
14.55pm:Ni wazi kwamba kocha mpya Jurgen Klopp hupiga mpira akiwa katika eneo lake alilokaa
14.45pm:Mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham imeanza
Image captionJurgen Klopp
14.00pm-Mechi ya Kwanza kwa Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool tangu iachukue klabu hiyo kutoka kwa alikuwa meneja Brendan Rodgers.
Mechi za ligi kuu ya Uingereza Jumamosi
Tottenham v Liverpool 2:45pm
Chelsea v Aston Villa 5:00pm
Crystal Palace v West Ham 5:00pm
Everton v Man Utd 5:00pm
Man City v Bournemouth 5:00pm
Southampton v Leicester 5:00pm
West Brom v Sunderland 5:00pm
Watford v Arsenal 7:30pm
Newer Post Older Post Home