Ziara za Wagombea nafasi za Urais kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania bado zinaendelea, Vyama vinaendelea kubadilishana Majukwaa ya Kampeni Mkoa kwa Mkoa.
Kwa upande wa Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. John Magufuli October 12 2015 ilikuwa ni zamu ya Lindi, katika Viwanja vya Sokoni Majengo.
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mama Salma Kikweteakihutubia wakazi wa Lindi mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za uliofanyika kwenye viwanja vya Mpilipili.
Mgombea ubunge jimbo la Mtama, Nape Nnauye akihutubia mbele ya Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCMuliofanyika kwenye viwanja vya Sokoni Majengo