LORI LAANGUKA NA KUZIBA BARABARA MUHIMU NAIROBI.

By | 23:08


Ajali
Image captionBarabara ya Uhuru Highway hutumiwa kuingia jiji la Nairobi ukitokea upande wa Westlands
Msongamano mkubwa wa magari umeshuhudiwa katika moja ya barabara kuu za kuingia jiji la Nairobi baada ya lori kuanguka na kufuziba upande mmoja wa barabara.
Wengi wa wakazi waliokuwa wakijiandaa kwenda kazini kutumia barabara hiyo ya Uhuru Highway karibu wamelazimika kutumia muda mwingi kufika jijini.
Ajali hiyo ilitokea usiku mita chache baada ya kupita mzunguko wa barabara wa Museum Hill ukielekea Nairobi.
Ajali
Image captionLori hilo lilikuwa limebeba mahindi
Magari yanayotaka kuingia jijini yanaelekezwa kutumia barabara ya Kijabe Street, mwandishi wa BBC Bashkas Jugsoday anasema.
Eneo hilo liko karibu na chuo kikuu cha Nairobi.
Ajali
Image captionFoleni ndefu ya magari imeshuhudiwa katika barabara hiyo
Hakuna ripoti zozote za majeruhi.
Barabara hiyo hutumiwa na watu wanaotoka maeneo ya magharibi mwa jiji na pia magharibi mwa nchi kama vile Naivasha na Nakuru, Eldoret na Kisumu.
Newer Post Older Post Home