Toka mshiriki wa BBAHotshots kutoka Tanzania, Idris ametangazwa kuwa mshindi, mengi yamekuwa yakisikika wengine wakihisi kuna tofauti kati ya Idris na mshiriki mwenzake ambaye waliingia fainali ambaye alikuwa mwakilishi wa Nigeria, Tayo.
Leo kupitia ukurasa wake wa Twitter (@IdrisSultan) ameandika ujumbe kuonyesha hakuna tofauti wala ugomvi wowote kati yake na Tayo ambaye alikuwa mwakilishi wa Nigeria ambaye walifanikiwa kuingia hatua ya fainali na Idris.
“Some people should just shut up about @Tayofaniran and me because clearly the problem is you, you’re busy crying while we living big. MOVE ON“– @IdrisSultan