Duniani kuna mambo…Hii imetokea huko Canada baada ya Mbwa kumpa maumizu ya moyo mmiliki wake kufuatia kuteketeza nyumba wakati akichezea kiberiti.
Wakizungumzia tukio hilo kikosi cha zima moto cha nchini humo kilisema moto ulianza kama masihara katika mji wa Mount Lorne wakati mbwa huyo akichezea box hilo la kiberiti kwa kulitafuna.
Uchunguzi ulibainika hakukua na mtu ama mbwa aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo kutokana na mmiliki huyo kuwa mbali lakini umeleta hasara kubwa ndani ya nyumba hiyo na ulizimwa baada ya kikosi hicho kuwasili kwenye tukio.