IFAHAMU TIMU YA ENGLAND YENYE MASHABIKI WENYE KELELE ZAIDI KULIKO WOTE.

By | 09:26
                      united fans
Utafiti uliofanyika kwenye timu za soka nchini England ukiwaangalia mashabiki wa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo umeonyesha klabu ambazo zina mashabiki wanaozipenda klabu zao kuliko wote.
Utafiti huo umeitaja Man United kuwa klabu ambayo mashabiki wake wanashangilia kwa kelele nyingi
kuliko mashabiki wote hususan kwenye mechi za ugenini .
Pamoja na kutokuwa na mengi ya kushangilia baada ya timu yao kutofanya vizuri tangu alipoondoka kocha Sir Alex Fergusson bado mashabiki wa United wametajwa kuwa na sauti kubwa kuliko wapinzani  wao kwenye mechi za ugenini .

                         Mashabiki wa Liverpool wanawafuatia mashabiki wa United kwa kelele nyingi kwenye mechi za ugenini .
Mashabiki wa Liverpool wanawafuatia mashabiki wa United kwa kelele nyingi 
kwenye mechi za ugenini .
Utafiti huu umeonyesha kuwa mashabiki wa United wanawazidi mashabiki wa
timu za Newcastle United na Liverpool ambao wanafuatia kwenye nafasi ya pili
na ya tatu kwa kelele zao wakati wakiwa wamesafiri kuitazama timu yao ugenini .
Klabu ya Arsenal imeshuka hadi nafasi ya saba hali ambayo huenda ikawa inachangiwa
kwa kiwango kikubwa na mashabiki wa timu hiyo kuonekana wamemchoka kocha wao
Arsene Wenger ambaye hivi karibuni alionekana hakubaliki mbele ya mashabiki wa timu
yake kiasi cha kutengeneza mabango ya kutaka aachie ngazi .
                            Mashabiki wa WestBrom  ndio wenye kelele chache kuliko mashabiki wote kwenye ligi kuu ya England .
Mashabiki wa WestBrom ndio wenye kelele chache kuliko mashabiki wote kwenye
 ligi kuu ya England .
Mashabiki wa timu zinazopambana kuepuka kushuka daraja kama vile Burnley na
Queens Park Rangers kwa pamoja na west Bromwich Albion zimeoneka kuwa na
 mashabiki wasio na kelele wanapokuwa kwenye mechi za ugenini hali ambayo
huenda ikawa inachangiwa na jinsi ambavyo timu zao zimeshindwa kupata matokeo
mazuri ziwapo ugenini .
Newer Post Older Post Home