MAAJABU HAYAISHI DUNIANI:AOMBA AZIKWE NA MBWA WAKE ATAKAPOFARIKI.

By | 23:32



Kutokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa mbwa wake huyo, huenda aliona kama iwapo atatangulia kufariki mbwa wake hatopata upendo kama anaompatia yeye.
Akiwa hai aliomba kama ikitokea yeye akafariki kabla ya mbwa wake basi wazikwe pamoja.
Mwanamke huyo Connie Lay raia wa Indian, Marekani aliyefariki siku chache zilizopita aliacha ombi hilo kwa rafiki zake, atakapokufa yeye na mbwa wake wazikwe pamoja, baada ya kufariki marafiki hao walituma ombi hilo kwa maafisa wanaoshughulikia haki za wanyama ambao walipinga ombi hilo.
Mbwa huyo aliyepewa jina la Bella, Lay alitaka azikwe naye ambapo ombi hilo lilipingwa na watu wa haki za wanyama huku wengine wakitaka kujitolea kumlea mbwa huyo ili aepukane na adhabu hiyo ya kifo.
Newer Post Older Post Home