Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni
wa Marekani John Kerry, amelazwa katika Hospitali moja mjini Geneva,
baada ya kuvunjika mguu, katika ajali ya uendeshaji baiskeli kwenye
milima ya Alps, nchini Ufaransa.
Amefutilia mbali ziara yake ya bara Ulaya na sasa atarejea nchini Marekani leo Jumatatu.John Kerry akipeleka baiskeli katika milima ya Alps nchini Ufaransa
Bwana Kerry alikuwa ziarani Switzerland kwa mazungumzo kuhusiana na mpango wa nuklia wa Iran, lakini akaamua kwenda mapumziko kidogo ya kuendesha baiskeli katika milima ya Alps, na hapo ndipo alipopata ajali hiyo.
Alipangiwa kuzuru Madrid leo Jumatatu.