Maafisa wa polisi nchini Kenya
wameanzisha uchunguzi kuhusu picha zilizowekwa katika mitandao ya
kijamii zinazoonyesha maafisa wa polisi wakiwachapa viboko raia wa
Somalia.
Takriban vijana kumi wameonekana wamelala ardhini huku polisi mmoja akiwawachapa viboko na mwingine akiwa ameshikilia bunduki.Waathiriwa hao wametambulika kama raia wa Somalia ambao wamevuka na kuingia nchini Kenya kupitia eneo la kazkazini mashariki mwa Kenya.
Picha hizo zilichapishwa katika mtandao wa facebook wa afisa mmoja wa polisi kutoka eneo hilo.
BBC SWAHILI.