Erdogan ataka kuwepo utulivu Uturuki
Rais
wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ametoa wito kwa vyama vyote vya
kisiasa Nchini humo, kufanya kazi pamoja na kuhakikisha kuwa kuna
mazingira mazuri ya kujiamini na kuleta utulivu kote Nchini humo.
Hotuba
yake inakuja baada ya matokeo ya ubunge kutangazwa hapo jana Jumapili
ambapo chama chake kilipata pigo kubwa kwa mara ya kwanza kwa kipindi
cha miaka kumi na mitatu iliyopita.Hakuna chama ambacho kimekubali kuunda serikali ya muungano.
Mwaandishi wa BBC Nchini Uturuki amesema kuwa chama cha AK huenda kikajaribu kuunda serikali ya wachache Bungeni, jambao ambalo si dhabiti.
Iwapo hakutakuwa na serikali itakayoundwa kwa kipindi ha siku arobaini na tano zinazokuja, hakutakuwa na jingine ila kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.