Mwenyekiti wa IPP DR Reginald Mengi ametunukiwa tuzo ya mjasiriamali mhamasishaji bora wa maendeleo kwa vijana.
Mwenyekiti
Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi ametunukiwa Tuzo ya Mjasiriamali
Mhamasishaji na Mchocheaji Bora wa Maendeleo kwa Vijana wa mwaka 2015.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi ametunukiwa Tuzo hiyo
jijini Dar es salaam na Chama cha Masoko cha Chuo Kikuu Dar es salaam
-DUMA, chenye uhusiano na Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu hicho,
wakati wa Tamasha la Masoko la mwaka huu, baada ya kuwashinda
wafanyabiashara Mohammed Dewji na Patrick Ngowi walioshindanishwa katika
kipengere hicho.
Rais wa DUMA Docta Ulimwengu amesema ushindi wa Dr Mengi na
washindi wengine wa tuzo hizo wamepatikana kwa kupigiwa kura na
wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu nchini.
Akipokea Tuzo hiyo Dr Mengi amewakumbusha vijana kuwa wamezungukwa
na fursa nyingi ambazo zinawahitaji wawe na macho yanayoweza kuona fursa
hizo ili waweze kuzitumia kujikwamua kiuchumi.
Wakati wa tamasha hilo, DUMA pia imewatunukia tuzo watu wengine
wanne ambapo mhe. Zitto Zuberi Kabwe alitunukiwa tuzo ya Mwanasiasa
Mhamasishaji Bora wa Vijana baada ya kuwashinda Mhe. Halima Mdee na Mhe.
January Makamba, na tuzo hiyo ilipokelewa kwa naiba yake na Prof.
Kitilya Mkumbo.
Aidha Bw. Sheria Ngowi alishinda Tuzo yaMwanamitindo Mhamasishaji
Bora kwa Vijana baada ya kuwashinda Jokate Mwigelo na Martin Kadinda.
Pia Mtangazaji Kijana Millard Ayo ametunukiwa Tuzo yaMwanahabari
Mhamasishaji Bora wa vijana ya kumshinda mtangazaji mwenzake Salama
Jabir.
Naye Mwanamuziki Diamond Platnum ametunukiwa tuzo ya Mwanamuziki
Mhamasishaji bora wa Vijana baada ya kuwashinda wanamuziki wenzake
Vanessa Mdee na Ali Kiba.
Tuzo za washindi hao zilipokelewa kwa niaba yao wawakilishi wao
baada ya wahusika kuwa nje ya jiji la Dar es salaam kwa sababu maalum.