Klabu ya Liverpool imetangaza
kufikia makubaliano na klabu ya Burnley juu
ya usajili wa mshambuliaji wa England Danny Inngs .
Liverpool ambayo msimu huu uliopita imejikuta
ikishindwa kufikia malengo yake baada ya kumaliza
nje ya nafasi za kufuzu michuano ya ligi ya mabingwa
imekuwa ikihaha kuhakikisha inasajili wachezaji ambao
wanaweza kuendana na malengo na ukubwa wa klabu
hiyo na Danny Inngs amekuwa kwenye orodha
ya kocha Brendan Rogers kwa muda mrefu .
Kinyume na hali ilivyokuwa kwa
klabu yake ya Burnley ambayo imeshuka
daraja Danny Inngs alikuwa na msimu mzuri
kwake binafsi akiwa ametokea kuwa moja
kati ya washambuliaji tishio kwenye ligi kuu
ya England baada ya kufunga mabao 11 .
Inngs pia alikuwa anatafutwa na klabu kadhaa
nchini England na barani ulaya ambapo kwa
nyakati tofauti Manchester United na Real
Sociedad ya Hispania zimekuwa zikihaha kusaka saini yake .
Ujio wa Ings huenda ukawa unamaanisha mwisho wa
washambuliaji Mario Balotelli na Rickie Lambert
ambao walishindwa kuonyesha ubora baada ya kusajiliwa msimu uliopita .
Related Items