Mwaka 1996 ndege ya Boeing 757 ilikuwa
imebeba abiria 189 ilipata hitilafu ikiwa ni dakika tano baada ya
kuondoka kufuatia kifaa cha kupima mwendo kasi wa ndege kuzibwa na kiota
cha nyuki hali iliyoleta taharuki kubwa miongoni mwa abiria.
Habari
inayofanana na hiyo imetokea huko Uingereza ambapo abiria walilazimika
kukaa kwa masaa mawili baada ya nyuki kuingia kwenye moja ya mitambo ya
injini za ndege hiyo na kutishia usalama wa abiri waliokua tayari
kuondoka.
Ndege hiyo inayoitwa Flybe yenye namba ya usajili BE384 iliyokuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin ikiwa na jumla ya abiria huku wahandisi walilazimika kutafuta mbinu ya kumtoa mdudu huyo.
Taarifa kutoka kwa shirika hilo lilisema
kuwa nyuki huyo alikuwa ndani ya mitambo muhimu ambayo ingehatarisha
maisha ya abiria wake wakiwa angani hivyo iliwalazimu kumtoa kwanza.
Related Items