TOTTENHAM KUMSAJILI MARTIAL WA UFARANSA.

By | 03:07





martial

Klabu ya Tottenham Hotspurs iko mbioni
kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji
wa As Monaco Anthony Martial baada ya
klabu hizo mbili kuanza mazungumzo huku
kukiwa na dalili kubwa za  kufikia makubaliano .
Martial ametokea kumvutia kocha wa Spurs
Mauricio Pochettino kwa kiwango alichoonyesha
msimu huu na amefunga mabao 8 katika michezo
zaidi ya 20 ya ligi ya Ufaransa huku akiiongoza Monaco
 kufika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa .
Martial ana umri wa miaka 19 na hii inamaanisha kuwa
bado ana mengi ya kujifunza huku kukiwa na uwezekano
wa kuongezeka kwa kiwango na thamani yake katika soko la
usajili na Spurs huenda ikapata faida kubwa endapo itaamua
 kumuuza hapo baadae .
Pamoja na hayo Pochettino huenda akawa anamsajili Martial
kama mbadala wa mshambuliaji Harry Kane ambaye tayari
 ameanza kuwaniwa na baadhi ya klabu kubwa nchini England
 ikiwemo Manchester United ambao wamekuwa
wakihusishwa na usajili wake .
Anthony Martial amefunga mabao 8 kwenye msimu huu wa ligi ya Ufaransa .
Anthony Martial amefunga mabao 8 kwenye msimu huu wa ligi ya Ufaransa .
Spurs kwa miaka mingi imekuwa klabu ambayo inauza wachezaji kwa timu
kubwa hali ambayo imewafanya wawe tayari kwa kusaka wabadala .
Katika miaka ya hivi karibuni Spurs imewauza Luka Modric , Gareth Bale ,
 Dimitar Berbatov na Michael Carrick huku kiwa tayari kusajili wachezaji
wengine kujaza mapengo yao.
Newer Post Older Post Home