Zikiwa zimepita siku tano pekee tangu
Rafael Benitez alipotambulishwa kuwa
kocha mpya wa Real Madrid kufuatia
klabu hiyo kumfukuza kazi Mtaliano
Carlo Ancelotti , tayari kocha huyu mpya ameanza
kutunishiana misuli na uongozi wa klabu hii ya kifalme
yenye maskani yake katikati ya mji mkuu wa Hispania .
Rafael Benitez kwa mujibu wa ripoti zilizoibuka hii leo
ametofautiana maoni na bosi wake ambaye ni rais wa
klabu hiyo Florentino Perez juu ya mshambuliaji
atayaesajiliwa na klabu hiyo ili kuimairisha kikosi
chake cha msimu wa mwaka 2015/2016.
Gazeti moja la kila siku nchini Hispania la habari za
michezo limeripoti kuwa Rafael Benitez anataka
kumrudisha mshambuliaji aliyeuzwa toka
Madrid Alvaro Morata baada ya kuridhishwa
na kiwango alichokionyesha msimu huu .
Matamanio haya ya Benitez kumsajili Alvaro
Moratta yanakwenda kinyume na Perez
ambaye anataka kumsajili Sergio Aguerro
ili aweze kuiongoza safu ya mashambulizi ya
Real Madrid kwa ajili ya msimu ujao .
Perez amekuwa na utamaduni wa kusajili wachezaji
nyota wenye majina makubwa kwa karibu kila msimu
ili kuifanya klabu hiyo itengeneze fedha kutokana na
biashara inayofanyika nje ya uwanja .
Florentino Perez na kocha mpya Rafa Benitez wameripotiwa kutofautiana
juu ya mshambuliaji wa kumsajili.
juu ya mshambuliaji wa kumsajili.
yoyote kwenye ufanyaji kazi wa Rafa Benitez lakini itakuwa ishara ya
kwanza ya aina ya mazingira ambayo anatajia kuyakuta akiwa
ameanza kazi rasmi kama kocha wa moja kati ya klabu kubwa kuliko zote duniani .
Related Items