Picha 6 za jumba la Asamoah Gyan lenye thamani ya bil 6
Asamoah Gyan ni mmoja wa
wachezaji wanaolipwa vizuri
kutoka katika bara la Afrika,
na hakuna uthibitisho mzuri wa
kuonyesha ukubwa wa malipo
yake zaidi ya ili hii mali mpya
alionunua, jumba kubwa la kifahari.
Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ain
ambaye analipwa kiasi cha $200,000
kwa wiki amenunua jumba hilo lenye
thamani inayokadiriwa kufikia dola millioni
3 za kimarekani ambazo zinafikia billioni 6 za kitanzania.
Jumba hilo lipo maeneo ya McCarthy Hills enclave
jijini Accra lina baa mbili, bwawa kubwa la kuogelea.
Lina ghorofa tatu zilizotengenezwa kwa muundo wa kipekee
kila mmoja huku vifaa vya ulinzi vikiwa vya kisasa ikiwepo
milango na madirisha yenye bullet proof.
Kwa mujibu taarifa za vyombo vya habari vya Ghana, Gyan
aliinunua nyumba hiyo aliyoikarabati alipozuru nchini humo
mwezi April wakati alipoenda kutazama pambano la
masumbwi kati Emmanuel Tagoe na Jobert Delos Reyes.