XAVI KWENYE KUAGWA HAKUWEZA KUZUIA HUZUNI YAKE.

By | 03:31


XAVI4
 Kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Barcelona dhidi ya Juventus, kiungo Xavi mwenye umri wa miaka 35 alipewa heshima katika klabu ambayo aliitumikia kwa muda mrefu tangu ana umri wa miaka 11 alipojiunga nayo.
XAVI
Fainali hiyo inayosubiriwa na watu wengi itafanyika siku ya Jumamosi.
Xavi ameshindwa kuzuia hisia zake na kumwaga machozi wakati wa shamrashamra za kumuaga ndani ya klabu yake ya Barcelona kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus.
XAVI2
Xavi amemshukuru kocha Luis Enrique kwa kumuwezesha kubaki katika klabu hiyo msimu uliopita huku akishindwa kuvumilia maneno ya Iniesta aliposimama na kumuaga kwa niaba ya wachezaji wenzake.
XAVI3
Kiungo huyo alitangaza mwezi uliopita kwamba anakwenda kumalizia soka yake katika klabu ya Al-Sadd ya Qatar mwishoni mwa msimu, akihitimisha miaka yake 24 kuwa na vigogo hao.
XAVI6
Newer Post Older Post Home